1 John 4

1Wapendwa, msiiamini kila roho, lakini zijaribuni roho muone kama zinatokana na Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani. 2Kwa hili mtamjua Roho wa Mungu - kila roho itakayokiri kuwa Yesu Kristo amekuja katika mwili ni ya Mungu, 3na kila roho isiyomkiri Yesu si ya Mungu. Hii ni roho ya mpinga kristo, ambayo mliyoisikia kuwa inakuja, na sasa tayari iko duniani.

4Ninyi ni wa Mungu, watoto wapendwa, na mmekwisha washinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu. 5Wao ni wa ulimwengu, kwa hiyo wanachokisema ni cha ulimwengu, na ulimwengu unawasikiliza. 6Sisi ni wa Mungu. Yeye amjuaye Mungu hutusikiliza sisi. Yeye asiye wa Mungu hawezi kutusikiliza. Katika hili tunajua roho wa kweli na roho wa uongo.

7Wapendwa, tupendane sisi kwa sisi, kwa vile upendo ni wa Mungu, na kila mmoja apendaye amezaliwa na Mungu na kumjua Mungu. 8Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo.

9Katika hili pendo la Mungu lilifunuliwa miongoni mwetu, kwamba Mungu alimtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni ili tuishi kupitia yeye. 10Katika hili pendo, si kwamba tulimpenda Mungu, lakini yeye alitupenda, na akamtuma Mwanawe awe fidia ya dhambi zetu.

11Wapendwa, ikiwa Mungu alitupenda sisi, vile vile tunapaswa kupendana sisi kwa sisi. 12Hakuna hata mmoja aliyemuona Mungu. Kama tukipendana sisi kwa sisi, Mungu anakaa ndani yetu na pendo lake limekamilika ndani yetu. 13Katika hili tunajua kuwa tunakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa Roho wake. 14Na tumeona na kushuhudia kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa mwokozi wa ulimwengu.

15Kila anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anakaa ndani yake na yeye ndani ya Mungu. 16Na tunajua na kuamini upendo alio nao Mungu ndani yetu. Mungu ni pendo, na yeye anayekaa ndani ya upendo anakaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.

17Katika pendo hili limekwisha kamilishwa kati yetu, ili tuwe na ujasiri siku ya hukumu, kwa sababu kama yeye alivyo, na sisi ndivyo tulivyo katika ulimwenngu huu. 18Hakuna hofu ndani ya pendo. Lakini pendo kamili huitupa hofu nje, kwa sababu hofu huhusiana na hukumu. Lakini yeye aogopaye hajakamilishwa katika pendo.

19Tunapenda kwa sababu Mungu alitupenda kwanza. 20Ikiwa mmoja atasema, “Nampenda Mungu” lakini anamchukia ndugu yake, ni mwongo. Kwa sababu asiyempenda ndugu yake, anayemuona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamuona. Na hii ndiyo amri tuliyo nayo kutoka kwake: Yeyote ampendaye Mungu, anapaswa kumpenda ndugu yake pia.

21

Copyright information for SwaULB